SCOTTLAND-USALAMA

Scottland: Watu kadhaa wajeruhiwa katika shambulio Glasgow

Katika eneo la shambulio huko Glasgow, Juni 26.
Katika eneo la shambulio huko Glasgow, Juni 26. @JATV_SCOTLAND/via REUTERS

Polisi ya Scottland imetangaza kwamba imefanikiwa kumuua mshambuliaji katika shambulio lililotokea Ijumaa huko Glasgow ambapo watu sita wamejeruhiwa, pamoja na afisa wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

"Polisi imemuangamiza mshambuliaji. Watu wengine sita wamejeruhiwa na kwa sasa wanapewa huduma hospitalini, akiwemo polisi mmoja ambaye yuko katika hali mbaya lakini madaktari wanajaribu kuweka hali yake sawa, "afisa wa polisi wa Scottland Steve Johnson amesema kwenye mtandao wa Twitter.

Hata hivyo vituo vya habari vya Sky News na BBC vimebaini kwamba watu watatu wameuawa katika tukio hilo huko Glasgow.

Waziri wa Mambo ya Ndani Priti Patel ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter habari "ya kutisha", bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Waziri Mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon ameelezea kisa cha Glasgow kama "tukio la kutisha".

Kulingana na Polisi, afisa wa polisi amechomwa kisu katika tukio hilo.

Kulingana na BBC watu watatu wamepoteza maisha.Tukio hilo linakuja siku sita baada ya vifo vya watu watatu katika shambulio la kisu huko Reading, shambulio lililodaiwa na polisi wa Uingereza kama la kigaidi.