UFARANSA-FILLON-HAKI

François Fillon ahukumiwa kifungo cha miaka 5

François Fillon na mke wake Pénélope walipofika kwenye mahakama ya Paris,  Juni 29, 2020.
François Fillon na mke wake Pénélope walipofika kwenye mahakama ya Paris, Juni 29, 2020. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa François Fillon na mke wake Pénélope, wamehukumiwa jela miaka mitano baada ya kupatikana na kosa katika kesi ya kughusi ajira.

Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo aliyehudumu kama Waziri Mkuu kati ya mwaka 2007 hadi 2012 chini ya rais Nicolas Sarkozy, alipatikana na kosa hilo baada ya kumlipa mkewe Dola 938,000 kwa kazi ambayo hakufanya kama msaidizi wake.

Jaji akitoa hukumu hiyo, amesema kuwa nafasi ya msaidizi aliyopewa mke wa Waziri huyo wa zamani haikustahili na hivyo alilipwa fedha kwa kazi ambayo hakufanya na hivyo, yalikuwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Licha ya kupewa kifungo cha miaka mitano jela, hata hivyo atatumikia kifungoi cha miaka mitatu nje ya jela.

Baada ya hukumu hiyo, wawili hao kupitia kwa Mawakili wao wamesema kuwa watakaa rufaa kuoinga kifungo hicho.

Fillion ambaye harakati zake za kuwania urais zilikatizwa kutokana na kashfa hii ya ufisadi, anakuwa kiongozi wa kwanza wa juu kupewa adhabu hiyo tangu kuundwa kwa Jamhuri ya tano mwaka 1958.