HUNGARY-EU-CORONA-AFYA

Hungary yakataa orodha ya nchi salama za EU

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban. REUTERS/Bernadett Szabo

Waziri Mkuu wa Hungary amekataa kufungua mipaka ya nchi yake kwa raia wa mataifa ambayo wiki hii Umoja wa Ulaya ulisema ni salama (hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha), isipokuwa raia kutoka Serbia.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya, ambao mipaka yake ya nje ilifungwa kama sehemu ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, ilifungua tena mipaka yao kuanzia Julai 1 kwa raia kutoka nchi 14 ambazo hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

Nchi hizo ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Moroccoo, New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay.

"Kwa sasa, hatuwezi kukubali ombi la Umoja wa ulaya (...) kwa sababu itakuwa ni kinyume na masilahi ya kiafya ya watu wa Hungary," amesema Viktor Orban katika video iliyorushwa kwenye mtandao wa Facebook.

Urusi na Brazil, kama ilivyo Marekani, hazikukidhi vigezo vya mataifa yaliyo salama kutokana na janga la Covid-19.