UFARANSA-SIASA

Serikali ya Edouard Philippe yajiuzulu

Waziri Mkuu Edouard Philippe akitoka ikulu ya Elysée, Oktoba 10, 2018.
Waziri Mkuu Edouard Philippe akitoka ikulu ya Elysée, Oktoba 10, 2018. Eric Feferberg / AFP

Waziri Mkuu wa Ufaransa Édouard Philippe amekabidhi barua ya kujiuzulu kwa serikali yake kwa Rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron, ambaye ameikubali, imetangaza ikulu ya Elysée, ambayo imesema katika taarifa kwamba waziri mkuu mpya "atateuliwa hivi karibuni".

Matangazo ya kibiashara

Mabadiliko haya ambayo yalipendekezwa na Rais Emmanuel Macron ambaye alitangaza kwamba "timu mpya" itaundwa ili kufuata "njia mpya" ya kisiasa kwa sehemu ya mwisho ya muhula wake hadi uchaguzi wa urais wa mwaka 2022.

Mabadiliko hayo yalipangwa kabla ya kufanyika uchaguzi, kwani serikali ya Macron imekuwa ikikosolewa wakati wa janga la virusi vya corona.

Mabadiliko hayo yanafanyika kufuatia uchaguzi wa manispaa wa Jumapili iliyopita, ambapo chama cha Kijani kilikishinda chama cha Macron katika miji mikubwa nchini humo.

Kulingana na Ikulu ya Elysee, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamchagua waziri mkuu mpya katika muda wa saa chache zijazo.