UFARANSA-SIASA

Ufaransa yampata Waziri mkuu mpya, baada ya Philippe kujiuzulu

Edouard Philippe na mrithi wake Jean Castex wakati wa kukabidhiana madaraka katika ofisi ya waziri mkuu, Matignon, Julai 3, 2020.
Edouard Philippe na mrithi wake Jean Castex wakati wa kukabidhiana madaraka katika ofisi ya waziri mkuu, Matignon, Julai 3, 2020. Thomas Samson, Pool via AP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mpya, kuchukua nafasi ya Edouard Philippe, aliyejiuzulu na Baraza lake la Mawaziri baada ya chama tawala kufanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa Castex, mwanasiasa wa upinzani anayeegemea siasa za mrengo wa kati, umewashangaza wengi ambao hawakutarajia rais Macron angefanya uteuzi huo.

Castex kabla ya kuteuliwa katika nafasi hii ya juu nchini humo amekuwa akiongoza Kamati inayosimamia mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona na kuoanekana kufanikiwa.

Baada ya uteuzi huu, anatarajiwa kutangaza baraza lake la Mawaziri, huku rais Macron akiahidi kuwa serikali yake mpya sasa itakuwa na mwelekeo mpya wa kuhakikisha kuwa taofa hilo linaimarika tena baada ya janga la Corona.

Wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa wanasema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, Rais Macron ameanza maandalizi ya mapema kwa kumteua mwanasiasa wa upinzani kuwa waziri mkuu, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuchagliwa tena.

Wakati alipopewa madarakani, Edouard Philippe, alionekana kupata umaarufu mkubwa kumpita rais Macron, licha ya serikali yake kushuhudia maandamano makubwa mwaka uliopita ya vizibao vya njano kupinga mageuzi ambayo walidai yanawapendelea matajiri.