UFARANSA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Jean Castex: Ufaransa haitafunga tena shughuli za maisha kitaifa

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex.
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex. REUTERS/Charles Platiau

Serikali ya Ufaransa, imesema imejipanga kukabiliana na mambukizi mapya ingawaje haina nia ya kusitisha shughuli za kawaida kutokana na hali iliyotokea siku za nyuma na kusababisha uchumi kuporomoka.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu mpya Jean Castex amesema  nchi hiyo imejifunza kutokana na amri ya awali ya kusitisha shughuli za kawaida ambayo imeathiri vibaya uchumi na maisha ya raia.

Bw. Castex amesema lengo lake ni kuianda Ufaransa kwa uwezekano wa wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya corona, wakati huo akilinda maisha ya kila siku ya kiuchumi na kijamii.

Ameyasema hayo baada ya kubaini kwamba kuna uwezekano wa kuongezekana kwa visa vya ugonjwa wa covid-19 katika miezi ijayo.