UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Uingereza: Bei ya ununuzi yaweza kupanda bila kuepo na mkataba wa kibiashara na EU

Kutoka kushoto kwenda kulia: Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. REUTERS

Sekta ya kibiashara ya Uingereza imetoa wito kwa Uingereza na Umoja wa Ulaya kufikia mkataba wa kibiashara wa baada ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo (Brexit).

Matangazo ya kibiashara

Sekta hiyo imebaini kwamba bila kuepo na mkataba wa ushuru, wanunuzi wanaweza kukabiliwa na ongezeko la bei kubwa mwaka ujao.

Sekta hiyo tayari imetangaza kupoteza maelfu ya ajira kufuatia janga la Corona, wakati wateja bado wanakosekana katika maduka licha ya masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona kuondolewa.

Mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita yameshindwa kuendelea, wakati tofauti kubwa zinaendelea kwa masuala kadhaa.

Uingereza ilijitoa rasmi katika Umoja wa Ulaya Januari 31, lakini inaendelea kuwa chini ya sheria za umoja huo wakati wa kipindi cha mpito hadi mwisho wa mwaka, hadi pande hizo mbili zitakapokubaliana juu ya uhusiano wao wa baadaye na wameepuka Uingereza kujitoa bila ya mkataba.