BOSNIA-MAUAJI-HAKI

Mauaji ya Kimbari: Waislamu wa Srebrenica wakumbuka ndugu zao waliouawa

Kufikia sasa, karibu miili 6,900 ya wahanga wa mauaji hayo iligunduliwa katika makaburi ya halaiki zaidi ya 80. Wengi wa wahanga hao wamezikwa kwenye eneo la makumbusho la mauaji ya kimbari huko Potocari.
Kufikia sasa, karibu miili 6,900 ya wahanga wa mauaji hayo iligunduliwa katika makaburi ya halaiki zaidi ya 80. Wengi wa wahanga hao wamezikwa kwenye eneo la makumbusho la mauaji ya kimbari huko Potocari. REUTERS / Dado Ruvic

Miaka 25 baadaye, Waislamu Srebrenic wanakumbuka mauaji ya ndugu zao waliouawa kikatili na vikosi vya Serb vya Bosnia. Mauji ambayo yalilaniwa na jumuiya ya kimataifa wakati huo.

Matangazo ya kibiashara

Ni mauaji mabaya kabisa yaliyotokea katika bara la Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Waislamu wa Bosnia wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica Jumamosi 11 Julai, ambap zaidi ya Waislamu 8,000 waliuawana jeshi la Bosnia.

Miaka ishirini na tano iliyopita, mnamo Julai 11, 1995, zaidi ya watu 8,000 kutoka jamii Waislamu wa Bosnia waliuawa katika mji wa Srebrenica na vikosi vya Serb vya Bosnia.

Maadhimisho rasmi yatafuatwa na mazishi ya mabaki ya wahanga tisa wa mauaji hayo. Mabaki yao yatazikwa kwenye makaburi yaliyotengwa kwenye eneo la makumbusho la mauaji ya kimbari huko Potocari, kijiji kinachopatikana karibu na Srebrenica ambapo kambi ya jeshi la Ulinzi la Umoja wa Mataifa (Forpronu) ilikuwa wakati wa vita vya kikabila vya Bosnia (1992-1995).

Kufikia sasa, karibu miili 6,900 ya wahanga wa mauaji hayo iligunduliwa katika makaburi ya halaiki zaidi ya 80. Wengi wa wahanga hao wamezikwa kwenye eneo la makumbusho la mauaji ya kimbari huko Potocari.

Hata hivyo wataalam wanasema miaka 25 baada ya mauaji ya Srebrenica mahakama za kimataifa kama ile iliyowahukumu waliofanya mauaji zinakabiliwa na hali isiyofahamika ya baadaye lakini zinahitajika kuliko wakati mwingine.