UFARANSA-SIASA-UCHUMI-JAMII

Castex atangaza uwekezaji wa Bilioni 6 katika mfumo wa utunzaji wa afya

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex akitoa hotuba kuhusu sera za jumla mbele ya Bunge Jumatano Julai 15.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex akitoa hotuba kuhusu sera za jumla mbele ya Bunge Jumatano Julai 15. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex amesema leo Jumatano mbele ya Bunge kwamba vita dhidi ya ukosefu wa ajira na utunzaji wa ajira vitakuwa "kipaumbele cha serikali kwa kipindi cha miezi 18 ijayo".

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex ametangaza mpango wa uwekezaji wa euro Bilioni sita katika mfumo mzima wa huduma za afya, kiwango ambacho kinakuja kuongezwa kwenye euro Bilioni 13 kama deni za hospitali, mfumo ambao tayari umepangwa na serikali.

"Lengo ni kutoa urahisi zaidi kwa vituo vya afya, kuingiza ubora wa utunzaji katika sheria za kufadhili hospitali na madaktari " na "kuzingatia kuzuia," amesema Waziri Mkuu wa Ufaransa katika hotuba yake ya sera za jumla.

Amesema kuwa "dharura ya kwanza" itakuwa vijana, "ambao ndio wa kwanza walioathiriwa na mgogoro uliosababishwa na janga la Covid-19" na kwamba mpango wa vijana "utajadiliwa Ijumaa wiki hii na wadau mbalimbali".

Serikali itasaidia hasa "kwa mpango wa kipekee kupunguza gharama ya kazi, hadi euro 4000 kwa mwaka, kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 25, hadi mara 1.6 mshahara wa chini, katika kampuni zote na kwa muda wa angalau mwaka mmoja".

Bw. Castex amesema matarajio ya kwanza ya serikali yatakuwa kuifanya upya Ufaransa"

"Matarajio yetu makubwa ya kwanza" yatakuwa "kupatanisha raia tofauti wa Ufaransa, kuboresha maridhiano kati ya wananchi wa taifa hili," amesema Waziri Mkuu Jean Castex Jumatano wakati wa hotuba yake kuhusu sera za jumla mbele ya Bunge.