UFARANSA-SIASA-UCHUMI-JAMII

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex kuzungumzia sera za jumla za serikali mbele ya Bunge

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Jean Castex katika Ikulu ya Elysée Julai 7, 2020.
Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Jean Castex katika Ikulu ya Elysée Julai 7, 2020. AP Photo/Francois Mori

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex anatarajia leo Jumatano kufafanua zaidi mbele ya wabunge mpango wa serikali uliotangazwa siku moja kabla na Rais Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Jean Castex atatangaza sera ya serikali, siku 12 baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Hakuna tofauti na kauli ya Rais Macron kwa aliyozungumzia Jumanne wiki hii katika mahojiano na waandishi wa habari, lakini Waziri Mkuu Jean Castex atatoa "njia mpya" kwa "kuwalinda raia wa Ufaransa" dhidi ya mdororo wa kiuchumi na kijamii, baada ya mgogoro wa kiafya ambayo umesababisha nchi hiyo inakabiliwa na mlipuko wa ukosefu wa ajira na kushuka kwa uchumi kwa 9 %.

Kwa hivyo Jean Castex anatarajiwa hasa katika utekelezaji wa mpango wa kuokoa uchumi, baada ya Rais Macron kuahidi "angalau euro Bilioni 100" zitakazotengwa kwa mpango huo, lakini ajira kwa vijana ndio ilipewa kipaumbele.

Waziri Mkuu anatarajia pia kuelezea jinsi serikali yake inaazimia "kutoa ushirikiano wake na serikali za mitaa", kulingana na matakwa ya Rais, na labda kutangaza uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Mipango serikali.

Jean Castex anatarajia kutetea tena haja ya mageuzi ya pensheni, kuanzia Ijumaa baada ya mkutano mpya na wadau mbalimbali; rais wa jamhuri anatarajia kutoka kwake 'ajenda inayofaa' ili kuweka sawa mageuzi hayo.