UFARANSA-EU-CORONA-UCHUMI

Macron: Nina matumaini lakini niko makini

Mkutano wa Baraza la Ulaya huko Brussels, 12 Desemba 2019.
Mkutano wa Baraza la Ulaya huko Brussels, 12 Desemba 2019. REUTERS/Yves Herman/Pool

Baraza la Ulaya ambalo linakutana leo Ijumaa kujadili bajeti ya mwaka ujayo ya Umoja wa Ulaya na mpango wa kurejesha uchumi wa euro bilioni 750 kukabiliana na janga la Covid-19 ni "wakati wa ukweli" kwa Ulaya, amesema rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipowasili jijini Brussels.

Matangazo ya kibiashara

"Huu ni wakati wa ukweli na matarajio kwa Ulaya," rais wa Ufaransa amesema mbele ya waandishi wa habari.

"Tunakabiliwa na afya isiyokuwa ya kawaida, lakini pia matatizo ya kiuchumi na kijamii, yanahitaji mshikamano zaidi na matarajio", ameongeza rais Macron.

"Saa kadhaa zijazo zitakuwa ni zenye maamuzi kwa kutimiza matarajio haya (...) Ni mradi wetu wa Ulaya ambao upo kwa faida ya wengi. Nina matumaini lakini ninaendelea kuwa makini (...) tutafanya kilio chini ya uwezo wetu ili tufikiye mkataba."

Wakuu wa nchi na serikali kutoka nchi 27 wanakutana kuanzia leo Ijumaa Julai 17 hadi kesho Julai 18. Ni kwa mara ya  kuanza viongozi hao watakutana ana kwa ana tangu kuibuka kwa janga hili la Corona.