EU-CORONA-UCHUMI

Viongozi wa EU washindwa kuafikiana kuhusu namna ya kuimarisha uchumi wa nchi zao

Hadi kufikia Jumatatu asubuhi, viongozi hao 27 chini ya rais wa Umoja huo Charles Michel wameshindwa kukubaliana kuhusu namna ya kugawana fedha hizo, huku maoni yakigawanyika iwapo fedha hizo zitolewe kama mkopo au msaada.
Hadi kufikia Jumatatu asubuhi, viongozi hao 27 chini ya rais wa Umoja huo Charles Michel wameshindwa kukubaliana kuhusu namna ya kugawana fedha hizo, huku maoni yakigawanyika iwapo fedha hizo zitolewe kama mkopo au msaada. FRANCOIS LENOIR / POOL / AFP

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya, wamekuwa katika mazungumzo ya muda mrefu kwa siku tatu, kutafuta mwafaka wa namna ya kugawana Euro Bilioni 750 fedha zinazotarajiwa kuimarisha uchumi wa nchi hizo kutokana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka Brussels zinasema kuwa wakati wa mazungumzo hayo, hasira zilipanda kati ya viongozi hao, huku tofauti za wazi zikioenkana kati ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na viongozi wa Uholanzi na Austria.

Hadi kufikia Jumatatu asubuhi, viongozi hao 27 chini ya rais wa Umoja huo Charles Michel wameshindwa kukubaliana kuhusu namna ya kugawana fedha hizo, huku maoni yakigawanyika iwapo fedha hizo zitolewe kama mkopo au msaada.

Wito wa mkuu huyo wa Umoja wa Ulaya kwa viongozi hao kuweka maslahi ya wananchi wao mbele ili kupata suluhu, unaonekana kutozaa matunda katika bara hilo ambalo limewapoteza watu zaidi ya Laki Mbili kutokana na janga la Corona.

Awali, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikuwa ameonya kuwa huenda mwafaka usipatikane, kutokana na mgawanyiko mkubwa kati ya viongozi wenzake kuhusu namna ya kugawana fedha hizo.