EU-CORONA-AFYA-UCHUMI

Nchi 27 za EU zafikia mkataba wa kufufua uchumi

Hatimaye viongozi wa Umoja wa Ulaya, baada ya mazungumzo ya siku nne,wamekubaliana namna ya kugawana zaidi ya Euro Bilioni 750 kuisaidia katika uimarishwaji wa uchumi wa nchi katika Umoja huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel baada ya kikao cha mwisho cha mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuhusu mpango wa kuinua uchumi, huko Brussels Julai 21, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel baada ya kikao cha mwisho cha mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuhusu mpango wa kuinua uchumi, huko Brussels Julai 21, 2020. STEPHANIE LECOCQ / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo ya siku nne, viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya walikuwa wakikutana kwa mazungumzo jijini Brussels hatimaye wamefikia mkataba Jumanne, Julai 21, kuhusu mpango wa kunusuru uchumi baada ya janga la Corona.

Viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya, EU, wamefikia mkataba Jijini Brussels Jumanne hii, Julai 21, mapema asubuhi, kuhusu mpango wa kihistoria wa kunusuru uchumi baada ya janga la Corona, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel ametangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Siku ya kihistoria kwa Umoja wa Ulaya," amepongeza Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye ukurasa wake wa Twitter, sekunde chache baada ya kutangazwa mkataba huo.

Mkutano huo uliowakutanisha viongozi wote wa nchi wanachama wa Umoja aw Ulaya ambao awali ulipangwa kufanyika saa 10:00 alaasiri uliahirishwa mara nyingi ili kuzingatia mahitaji ya kila mmoja. Na ulianza kabla ya saa 9:30 usiku.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na Euro Bilioni 390 kutolewa kama misaada kinyume na Euro Bilioni 500 iliyokuwa imetangazwa hapo awali.