UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yakaribia 207,000 nchini Ujerumani

Idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zilizothibitishwa nchini Ujerumani imepanda hadi 206,926, baada ya zaidi ya visa vipya 684 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita, kulingana na takwimu iliyotolewa leo Jumatano na Chuo Kikuu cha Robert Koch (RKI).

Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi.
Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vifo zaidi ya sita vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufikisha jumla ya vifo 9,128 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Jumanne wiki hii taasisi inayodhibiti magonjwa nchini humoinasema ilisema inahofia ongezeko la maambukizi ya Corona nchini Ujerumani, huku ikionya raia wake dhidi ya kusafiri katika baadhi ya majimbo nchini Uhispania.

Kiongozi wa taasisi hiyo Lothar Wieler, alisema kuwa maambukizi hayo ambayo yalionekana kupungua sasa yameanza kuongezeka tena, suala ambalo amesema linazua wasiwasi.

Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi.

Raia wa nchi hiyo sasa wametakiwa kuheshimu kanuni za Wizara ya Afya na kuhakikisha kuwa wanavalia barakoa kila wakati wanapokuwa nyumbani na maeneo mengine ya umma.

Hili ni onyo linalokuja wakati huu dunia ikishuhudia ongzeko la virusi vya Corona, huku Wizara ya Mambo ya Nje nchini Ujerumani ikiwataka raia wake kutoenda katika majimbo matatu Kaskazini mwa Uhispania, yanayoaminiwa kuendelea kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.

Ujerumani imekuwa ikisifiwa kwa kutoa huduma ya haraka kwa watu walioambukizwa katika taifa hilo, ambalo limeshuhudia vifo vya watu zaidi ya Elfu Tisa.