ULAYA-WHO-CORONA-AFYA

WHO yaonya kuhusu ongezeko la maambukizi kwa vijana Ulaya

Shirika la Afya duniani WHO linaonya kuwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa vijana barani Ulaya, ni tishio kubwa la kuongezeka kwa maambukizi hayo katika bara hilo.

ipoti zinasema kuwa vijana wengi wameendelea kukaidi ushauri ya kutokusanyana na kufanya sherehe au kwenda katika maeneo ya kitalii ili kuepuka maambukizi hayo.
ipoti zinasema kuwa vijana wengi wameendelea kukaidi ushauri ya kutokusanyana na kufanya sherehe au kwenda katika maeneo ya kitalii ili kuepuka maambukizi hayo. NEXU Science Communication/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge, amesema ongezeko la hivi karibuni limeonakana kwa vijana na viongozi wa mataifa mbalimbali wana jukumu la kuwasiliana ipasavyo  na vijana na kuwafikishia ujumbe kuhusu maambukizi ya Corona.

Aidha, amesema ongezeko hili linatokana na vijana wengi barani Ulaya ambao wameshindwa kubadilisha tabia zao hata baada ya kuzuka kwa janga hili.

Ripoti zinasema kuwa vijana wengi wameendelea kukaidi ushauri wa kutokusanyana na kufanya sherehe au kwenda katika maeneo ya kitalii ili kuepuka maambukizi hayo.

Hivi karibuni, serikali ya Uingereza iliwamiliza wananchi wa taifa hilo, hasa vijana kupunguza uzito kwa kubadilisha mfumo wao wa kula ili kusaidia katika mapambo dhidi ya janga hili.

Tangu kuzuka kwa maambukizi ya Corona mapema mwaka huu, bara la Uaya limeripoti visa zaidi ya Milioni mbili na vifo zaidi ya Laki Mbili.