Miili ya wafanyakazi sita wa shirika la misaada waliouawa Niger yawasili Paris
Imechapishwa: Imehaririwa:
Viongozi wa serikali ya Ufaransa wametoa heshima za mwisho kwa wafanyakazi sita wa shirika la misaada la ACTED, raia wa Ufaransa waliouawa nchini Niger na kundi la wahalifu.
Waziri Mkuu Jean Castex aameongoza sherehe hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Orly.
Familia, ndugu, jamaa na marafiki wa wahanga hao walihudhuria sherehe hiyo.
Waziri Mkuu, Jean Castex akiongozana na Waziri wa Sheria, Eric Dupond-Moretti na Jean-Baptiste Lemoyne, Katibu dola kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya nje, wamewakilisha serikali katika sherehe hiyo.
Watu wanane - Wafaransa sita na raia wawili wa Niger - waliuawa na watu wenye silaha ambao walikuja kwa pikipiki katika eneo la Kouré, Kusini Magharibi mwa Niger, eneo linalojulikana kama hifadhi ya mwisho ya Twiga huko Afrika Magharibi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Niger Mahamadou Issoufou waliapa kuendelea na vita dhidi ya makundi ya kijihadi hadi pale watahakikisha makundi hayo yametokomezwa.