UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 1,700 zathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. REUTERS

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virisi vya Corona nchini Ujerumani imeongezeka hadi 228,621, baada ya kesi mpya 1,707 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa na kituo cha udhibiti wa maradhi ya kuambukiza cha Robert Koch.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hii ni kubwa kuwahi kuripotiwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyotangulia.

Vifo vipya kumi vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufikisha jumla ya vifo 9,253 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.

Siku ya Jumanne wiki hii, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka.