UHISPANIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Baadhi ya wakazi wa mji wa Madrid watakiwa kubaki ndani, maambukizi yaongezeka Uhispania

Baada ya kukosolewa kwa ukosefu wa taarifa juu ya tarehe na utaratibu wa kuanza kwa mwaka wa shule, wizara ya elimu nchini Uhispania imetangaza kwamba haitawezeka mwaka wa shule kuanza mwezi Septemba.
Baada ya kukosolewa kwa ukosefu wa taarifa juu ya tarehe na utaratibu wa kuanza kwa mwaka wa shule, wizara ya elimu nchini Uhispania imetangaza kwamba haitawezeka mwaka wa shule kuanza mwezi Septemba. Community of Madrid/Handout via REUTERS

Mamlaka katika mji wa Madrid wameshauri wakazi wa maeneo yenye visa vingi vya COVID-19 kukabaki nyumbani, wakati wizara ya afya ya Uhispania ikiripoti zaidi ya maambukizi mapya 3,000 kwa siku ya nne mfululizo.

Matangazo ya kibiashara

Katika muda wa saa 24 zilizopita, kesi mpya 3,650 zimethibitishwa baada ya kufanya vipimo, na kufanya jumla ya kesi za maambukizi kufikia 386,054. Pamoja na kesi 1,199 za maambukizi, mji mkuu wa Uhispania, Madrid umerekodi karibu theluthi moja ya kesi mpya za maambukizi.

Antonio Zapatero, Naibu Waziri wa Afya ya Umma wa Comunidad de Madrid, amewataka wananchi wa taifa hilo kuepuka safari na mikutano isiyo ya muhimu, na amewataka wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa zaidi kubaki nyumbani, huku akikanusha kwa sasa kuwa serikali ina mpango wa kuchukuwa masharti mapya ya raia kutotembea.

Baada ya kukosolewa kwa ukosefu wa taarifa juu ya tarehe na utaratibu wa kuanza kwa mwaka wa shule, wizara ya elimu nchini Uhispania imetangaza kwamba haitawezeka mwaka wa shule kuanza mwezi Septemba.

Kwa jumla, janga hilo limeuwa watu 28,838 nchini Uhispania.

Katika kudhibiti mlipuko mpya, serikali ya Uingereza imeagiza kufungwa kwa sehemu za starehe za usiku, na kuchukua hatua kadhaa kwa mikahawa kufunguliwa. Waziri wa Usawa, Irene Montero pia amewataka viongozi wa mkoa wa Madrid kuchukua hatua za kufunga maeneo wanakokusanyika watu wengi, ambayo ni chanzo maambukizi.