UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya vya maambukizi vyapungua nchini Uingereza

Uingereza imerekodi visa lakini 3 na Elfu 23 vya maambukizi baada ya visa vipya 1, 033 kuthibitishwa. Watu 41 405 wamefariki dunia, baada ya vifo vipya 2 kuthibitishwa.
Uingereza imerekodi visa lakini 3 na Elfu 23 vya maambukizi baada ya visa vipya 1, 033 kuthibitishwa. Watu 41 405 wamefariki dunia, baada ya vifo vipya 2 kuthibitishwa. REUTERS/Toby Melville

Mamlaka nchini Uingereza imeripoti kesi mpya 1,033 za maambukizi ya virusi vya Corona katika saa 24 zilizopita, dhidi ya kesi mpya 1,182 siku iliyotangulia.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengine wawili wamefariki dunia katika muda wa siku 28 baada ya kupimwa na matokeo kuonyesha kuwa wameambukizwa virusi vya Corona, ikilinganishwa na vifo sita siku ya Alhamisi.

Mamlaka ya afya inabaini kwamba kiwango cha kukuwa kwa virusi ("R") nchini Uingereza sasa kinaweza kuwa juu ya 1, hali ambayo inaashiria hatari ya kuongeza kasi ya maambukizi.

Kiwango hiki kinakadiriwa kuwa kati ya 0.9 na 1.1, dhidi ya 0.8 hadi 1.0 wiki iliyopita.

Kiwango kikubwa kuliko 1 inamaanisha kuwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona anweza kuambukiza zaidi ya mtu mmoja kwa wastani.

Uingereza imerekodi visa lakini 3 na Elfu 23 vya maambukizi baada ya visa vipya 1, 033 kuthibitishwa. Watu 41 405 wamefariki dunia, baada ya vifo vipya 2 kuthibitishwa.