MAREKANI-EU-USHIRIKIANO

Marekani na Umoja wa Ulaya wafikia mikataba ya kupunguza baadhi ya kodi

Moja ya mikataba hiyo unapelekea kusitishwa kwa kodi ya 8% hadi 12% iliyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa baadhi ya vifaa muhimu kutoka Marekani na kupunguzwa kwa nusu ya kodi ya Marekani kwa bidhaa kutoka nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Moja ya mikataba hiyo unapelekea kusitishwa kwa kodi ya 8% hadi 12% iliyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa baadhi ya vifaa muhimu kutoka Marekani na kupunguzwa kwa nusu ya kodi ya Marekani kwa bidhaa kutoka nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya. REUTERS

Marekani na Umoja wa Ulaya wametangaza kwamba wamefikia mikataba ya kupunguza kodi kwa idadi ndogo ya bidhaa, ikiwa ni pamoja na moja ya bidhaa muhimu kutoka Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Pande hizi mbili pia zinaendelea kukabiliwa na mgogoro juu ya maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na lile la misaada ya umma kwa makampuni ya kutengeneza ndege na lile linalohusiana na adhabu

kuhusu chuma na aluminium kutoka Ulaya.

"Hata hivyo umuhimu wa mikataba hii ni kwamba imewezesha kupatakina kwa matokeo mazuri ," ofisa mmoja wa Umoja aw Ulaya amesema.

Moja ya mikataba hiyo unapelekea kusitishwa kwa kodi ya 8% hadi 12% iliyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa baadhi ya vifaa muhimu kutoka Marekani na kupunguzwa kwa nusu ya kodi ya Marekani kwa bidhaa kutoka nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mikataba hiyo iliyotangazwa siku ya Ijumaa inatarajiwa kuidhinishwa na serikali na bunge vya Umoja wa Ulaya, hali ambayo inaonekana itachukuwa wiki kadhaa.