UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 1,200 zathibitishwa Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. AFP/Torsten Silz

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imeongezeka hadi 234,853, baada ya kesi mpya zaidi ya 1,278 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa na kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya vitano vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya idadi ya vifo kufikia 9,277 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa Wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka.