UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 1,500 vya maambukizi vyathibitishwa Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. REUTERS

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imeongezeka hadi 236,429, baada ya kesi mpya 1,576 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumatano na kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kuambukia cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vingine vitatu vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,280 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini ujerumani.

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa Wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka.