UFARANSA-CORONA-AFYA-ELIMU

Ufaransa: Jean Castex atoa wito kwa 'uwajibikaji' juu ya uvaaji wa Barakoa

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex akitangaza wajibu wa kuvaa barakoa katika maeneo ya umma yaliyofungwa mbele ya  bunge la Seneti mnamo Julai 16, 2020.
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex akitangaza wajibu wa kuvaa barakoa katika maeneo ya umma yaliyofungwa mbele ya bunge la Seneti mnamo Julai 16, 2020. AFP Photo/Bertrand Guay

Sekta ya utamaduni itanufaika na "kiwango cha kipekee" cha euro Bilioni mbili katika mpango wa kuokoa bilioni 100 ambao utatangazwa Septemba 3, Waziri Mkuu wa Ufaransa ametangaza Jumatano kwenye redio ya umma ya France.

Matangazo ya kibiashara

Jean Castex pia ametoa wito kwa wananchi wa Ufaransa kuwa na "nyoyo za uwajibikaji" kwa kuvaa barakoa, jambo ambalo 'ni muhimu sana' katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19,.

Wakati huo huo Jean Castex amefutilia mbali hoja ya kuwapa bure barakoa wanafunzi wote nchini Ufaransa.

Baada ya kukataa kutoa bure barakoa katika shule mbalimbali nchini Ufaransa, Jean Castex alikuwa anatarajiwa kuweka wazi uamuzi huo uliozua utata.

"Siamini kuwa serikali inaweza kufanya kila kitu, kwa upande wake ina makumu ambayo inatakiwa kufanya [...], lakini sote pamoja tunatakiwa kuwajibika katika mapambano dhidi ya COVID-19, " amesema Waziri Mkuu wa Ufaransa.

Jean Castex amebaini kwamba hakuna nchi duniani iliyokubali kutoa barakoa bure kwa wanafunzi.. Hata hivyo amesema kuwa watu ambao wamedhoofika kiafya au kifedha wanaweza kupewa bure barakoa.

"Hatutanunulia barakoa familia ambazo haziitaji kabisa," amesisitiza Jean Castex, wakati uvaaji barakoa ni lazima kwa wanafunzi wa shule za upili na sekondari tangu kuanza kwa mwaka wa shule Jumanne ya wiki ijayo.