UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yaendelea kuongezeka nchini Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. Ina FASSBENDER / AFP

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imeongezeka hadi 237,936, baada ya zaidi ya kesi mpya 1,507 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu iliyotolewa leo Alhamisi na kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kuambukia ya Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya vitano vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya idadi ya vifo kufikia 9,285 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa Wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka.