UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yakaribia 240,000 Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. REUTERS

Idadi ya visa vilivyothibitishwa yvamaambukizi ya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 239,507, baada ya visa vipya 1,571 kuthibitishwa katika muda wa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kuambukia cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vingine vitatu vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufikisha jumla ya idadi ya vifo kufikia 9,888 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa Wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.