UFARANSA-CORONA-UCHUMI

Serikali ya Ufaransa kutangaza mpango wake wa kuinua uchumi

Waziri Mkuu Jean Castex anatarajia kufafanua kwa undani mpango mpya wa kuinua uchumi. Hapa, ilikuwa katika mkutano wa majira ya joto wa MEDEF, Agosti 26, 2020.
Waziri Mkuu Jean Castex anatarajia kufafanua kwa undani mpango mpya wa kuinua uchumi. Hapa, ilikuwa katika mkutano wa majira ya joto wa MEDEF, Agosti 26, 2020. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Baada ya mgogoro wa wa kiafya kutokana naCorona na hatua za kukabiliana na ugonjwa huo, serikali ya Ufaransa inatarajia leo Alhamisi kutangaza mpango wake wa euro bilioni 100, unaoitwa "Ufaransa yazindua" na unakusudia, kwa mujibu wa Emmanuel Macron, "kuandaa Ufaransa ya mwaka 2030".

Matangazo ya kibiashara

Serikali inataka kufadhili kipindi cha miaka ijayo wakati ikishughulikia mgogoro wa sasa.

"Baada ya kipindi cha dharura, muda umewadia wa kufufua uchumi". Wasaidizi wa Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex wamebaini: mpango wake utawezesha uchumi wa Ufaransa kuongezeka tena. Na kufuta hasara iliyosababishwa na ugonjwa hatari wa Covid-129 ifikapo mwaka 2022.

"Usawazishaji" ni sahihi, ameongeza mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu. Euro bilioni 100 ni sawa na asilimia 4 ya pato la taifa yaliyopotea wakati wa mgogoro wa kiafya na bajeti ya nchi itaweza kuzikusanya, viongozi serikalini wameahidi.

Wazo la serikali ni kuwekeza katika sekta ambazo zitakuza uchumi katika miaka kumi ijayo. Vijana 200,000, kwa mfano, watapewa mafunzo katika taaluma za miaka ijayo kama haidrojeni au afya.

Ikiwa hiyo haitoshi? Ikiwa mpango huu utachelewa kutekelezwa, kama unavyodai upinzani kutoka mrengo wa kushoto? "Tuko tayari kurekebisha, na kuzoea," Ofisi ya Waziri Mkuu (Matignon) imebaini. Serikali italazimika kusonga mbele hatua kwa hatua dhidi ya mgogoro ambao unaweza kuwepo hadi uchaguzi wa urais ujao.