UHISPANIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia 498,989 nchini Uhispania

Idadi ya vifo nchini Uhispania, katika siku saba zilizopita ni 256, na kufanya jumla ya vifo kufikia 29,418.
Idadi ya vifo nchini Uhispania, katika siku saba zilizopita ni 256, na kufanya jumla ya vifo kufikia 29,418. REUTERS

Uhispania imerekodi visa vipya 4,503 vya maambukizi ya virusi vya Corona, dhidi ya 3,607 siku moja kabla, na hivyo kufanya jumla ya visa vya maaambukizi kufikia 498,989.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo katika siku saba zilizopita ni 256, na kufanya jumla ya vifo kufikia 29,418.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Nchi zilizoathirika zaidi na mgogoro wa kiafya kutokana na virusi vya Corona ni Marekani na Brazil.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, lilizitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona na kuonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.