UFARANSA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu kesi mpya 9,000 kwa siku moja zathibitishwa nchini Ufaransa

Mtu huyu akifanyiwa vipimo vya Covid-19 mbele ya makao makuu ya mji wa Paris Septemba 2, 2020.
Mtu huyu akifanyiwa vipimo vya Covid-19 mbele ya makao makuu ya mji wa Paris Septemba 2, 2020. Christian Hartmann/Reuters

Mamlaka ya afya inchini Ufaransa imebaini kwamba karibu kesi mpya 9,000 za Covid-19 zimeripotiwa Ijumaa nchini Ufaransa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni rekodi tangu kuzuka kwa janga hilo. raia wametakiwa kuwa makini kutokana na hali hiyo.

Kesi mpya 8,975 za Covid-19 zimethibitishwa katika muda wa saa 24 nchini Ufaransa, kulingana na takwimu zilizotolewa Ijumaa Septemba 4 na mamlaka ya Afya nchini humo.

Hii inawakilisha ongezeko la maambukizi ikilinganishwa na siku zilizopita. Jumatano na Alhamisi, kuliripotiwa zaidi ya kesi mpya 7,000 katika muda wa saa 24. Karibu kesi mpya 9,000: rekodi nchini Ufaransa tangu kuzuka kwa janga hilo hatari na uzinduzi wa vipimo vikubwa.

Italia iko tayari kusaidia Ufaransa

Ufaransa inaendelea kukumbwa na maambukizi mapya ya virusi vya Corona: visa vipya 53 pia vimethibitishwa. Kutokana na ongezeko la visa, Italia imesema iko tayari kusaidia Ufaransa. "Wakati mbaya zaidi wa janga hilo, Ufaransa haikufunga mipaka yake lakini ilisaidia Italia kwa vifaa vya usafi. Hatusahau kitendo hiki, ”Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Luigi Di Maio amesema.

Zaidi ya watu Milioni moja wamefanyiwa vipimo kaika muda wa siku saba zilizopita nchini Ufaransa. Hata hivyo idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona inaendelea kuongezeka. Ilifikia 4.5% jana Ijumaa, wakati siku ya Alhamisi ilikuwa chini ya 4.4%.

Wakati huo huo wagonjwa 473 wamelazwa hospitalini katika wodi ya wagonjwa mahututi, ikiwa ni pamoja na 46 katika muda wa saa 24 zilizopita. Wagonjwa wengine tisa wameongezeka kwenye idadi hiyo ikilinganishwa na takwimu ya Alhamisi.