EU-UTURUKI-UGIRIKI-USALAMA

Med7 yaunga mkono vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Uturuki ikiwa Ankara haishiriki mazungumzo

Emmanuel Macron anafungua mkutano wa Med7 na nchi zingine sita zinazopakana na bahari ya Mediterenia, Septemba 10, 2020.
Emmanuel Macron anafungua mkutano wa Med7 na nchi zingine sita zinazopakana na bahari ya Mediterenia, Septemba 10, 2020. Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Viongozi wa saba zinazopakana na bahari ya Mediterenia EuroMed7 ambao walikutana Alhamisi, Septemba 10 huko Corsica wametoa wito kwa Uturuki kushiriki mazungumzo na kutishia kuichulia vikwazo ikiwa Ankara itaendelea na "vitendo vyake vya uchokozi" katika bahari ya Mediterania.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo amesema kuwa taifa hilo mshirika wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, sio mshirika tena katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Mediterenia na kwamba raia wake wanastahili mambo tofauti kinyume na vile serikali hiyo inavyofanya kwa sasa.

"Viongozi wa nchi saba walitaka kurejelea mazungumzo na Uturuki kwa ''nia njema tu, lakini ikiwa Ankara itakataa kushiriki mazungumzo Umoja wa Ulaya hautochelewa kuichukulia vikwazo, '' amesema rais wa Ufaransa.

Taarifa ya mwisho ya viongozi hao ilionesha wazi kuwa vikwazo ni suala linalozingatiwa iwapao Uturuki itashindwa kumaliza ''vitendo vyake vya uchokozi.''

Mkutano huo katika kisiwa cha Ufaransa cha Corsica uliwaleta pamoja viongozi wa Ufaransa, Italia, malta, Ureno na Uhispania pamoja na wanachama wa Umoja wa Ulaya wa mataifa ya mashariki mwa bahari ya Mediterania, Ugiriki na Cyprus.

Ugiriki inaendelea katika mvutano na Uturuki kuhusiana na maliasili ya gesi na mafuta pamoja na ushawishi wa jeshi la majini katika eneo la Mashariki mwa Mediterania ambao umezusha hofu za mzozo.