UFARANSA-CORONA-AFYA

Madaktari watoa wito wa kukabiliana vilivyo na Corona Ufaransa

Mfanyakazi wa kilimo cha msimu afanyiwa vipimo vya Corona Juni 10 huko Chateaurenard, Kusini mwa Ufaransa.
Mfanyakazi wa kilimo cha msimu afanyiwa vipimo vya Corona Juni 10 huko Chateaurenard, Kusini mwa Ufaransa. CLEMENT MAHOUDEAU / AFP

Ufaransa kwa mara nyingine imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya watu wengine 10,561 kuambukizwa kwa muda wa saa 24 zilizopita Jumamosi Septemba 12.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni rekodi tangu kuzinduliwa kwa zoezi la upimaji mkubwa nchini Ufaransa. Takwimu zilizochapishwa siku ya Jumamosi, Septemba 12 mamlaka ya Afya ya Umma nchini Ufaransa zinaonyesha zaidi ya kesi 10,500 za maambukizi zilizothibitishwa kwa siku moja, dhidi ya karibu kesi 9,400 za maambukizi zilizoripotiwa siku ya Ijumaa.

Siku za hivi karibuni, Ufaransa imeshuhudia idadi kubwa ya maambukizi, hali inayozua wasiwasi.

Watu zaidi ya Elfu 30 wamepoteza maisha kutokana na janga hili nchini Rwanda tangu mwezi Machi.

Kiwango cha watu waliopatikana na virusi vya Corona, ni kusema idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo ikilinganishwa na jumla ya idadi ya watu waliopimwa, kwa upande mwingine, inabaki thabiti kwa 5.4% nchini kote.