ULAYA-WHO-CORONA-AFYA

WHO yaonya kuhusu kutokea kwa vifo vinavyohusiana na Corona

Shirika la Afya Duniani limetoa wito wa kukabiliana vilivo dhidi ya Corona.
Shirika la Afya Duniani limetoa wito wa kukabiliana vilivo dhidi ya Corona. REUTERS/Denis Balibouse/File Photo

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona, vinatarajiwa kuongeka kati ya mwezi Oktoba na Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge ametoa onyo hilo, licha ya kusema kuwa hivi karibuni, bara hilo limeshuhudia ongezeko la maambukizi lakini idadi ya vifo haijaongezeka sana.

Aidha, Kluge ameonya kuwa hata iwapo chanjo itapatikana, haitakuwa mwisho wa maambukizi hayo.

Bara la Ulaya lina maambukizi zaidi ya Milioni Mbili na vifo zaidi ya Laki Mbili.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.