EU-USHIRIKIANO-CORONA-

Mkutano wa Baraza la Ulaya waahirishwa hadi Oktoba 1 na 2, Charles Michel ajiweka karantini

Charles Michel hakupatikana na ugonjwa huo baada ya kufanya vipimo siku ya Jumatatu lakini anafuata sheria za kujiweka karantini zinazotumika nchini Ubelgiji, amesema msemaji wake.
Charles Michel hakupatikana na ugonjwa huo baada ya kufanya vipimo siku ya Jumatatu lakini anafuata sheria za kujiweka karantini zinazotumika nchini Ubelgiji, amesema msemaji wake. REUTERS

Mkutano wa Baraza la Ulaya, uliokuwa umepangwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa, umeahirishwa hadi 1 na 2 Oktoba, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, amejiweka kizuizini baada ya kutangamana wiki iliyopita na mtu aliye ambukizwa virusi vy Corona, msemaji wake amesema.

Matangazo ya kibiashara

Charles Michel hakupatikana na ugonjwa huo baada ya kufanya vipimo siku ya Jumatatu lakini anafuata sheria za kujiweka karantini zinazotumika nchini Ubelgiji, amesema msemaji wake.

Kufikia sasa ugonjwa wa COVID-19 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 966,000. Watu Milioni 31,4 wameambukizwa virusi vya Corona na Milioni 21,5 wamepona ugonjwa huo hatari.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.