UFARANSA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus-Ufaransa: Marufuku kuuza na kufungua mikahawa katika miji ya Marseiile na Paris

Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Véran, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, Septemba 23, 2020.
Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Véran, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, Septemba 23, 2020. AFP/POOL/Eliot Blondet

Ufaransa imeagiza kufungwa kwa vilabu vya kuuza pombe na mikahawa mjini Marseille na kudhibiti biashara hiyo katika maeneo ya jijini la Paris ili kusaidia kupambana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya nchi hiyo ya bara Ulaya kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona kuanzia mwezi Agosti na kutangaza kudhibiti mikusanyiko ya watu katika maeneo ya umma.

Ufaransa ina maambukizi zaidi ya Laki Nne na Elfu 80 na vifo zaidi ya elfu 31.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex pia alitoa wito kwa wananchi wa Ufaransa kuwa na "nyoyo za uwajibikaji" kwa kuvaa barakoa, jambo ambalo 'ni muhimu sana' katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19.