UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 2,100 zathibitishwa nchini Ujerumani

Ujerumani inaendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi.
Ujerumani inaendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi. AFP/Torsten Silz

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 278,070, baada ya kesi zaidi ya 2,143 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo zaidi ya 19 vimeripotiwa, kulingana na RKI, na kufikisha jumla ya vifo 9,428 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.