UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ujerumani yaondoa marufuku kwa safari za kigeni

Ujerumani imeondoa vikwazo vya safari za kigeni katika nchi ambazo si wanachama wa Umoja wa Ulaya, ilivyoweka dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19 tangu miezi sita sasa, ingawa mapendekezo mapya yanatarajiwa kuleta mabadiliko kidogo kwa wengi wa wasafiri.

Mwezi Machi mwaka huu Berlin ilikuwa imepiga marufuku safari zote, wakati virusi vilikuwa vikiendelea kaskazini mwa Italia, kabla ya kufungua mipaka yake kwa nchi nyingi za Ulaya mwezi Juni.
Mwezi Machi mwaka huu Berlin ilikuwa imepiga marufuku safari zote, wakati virusi vilikuwa vikiendelea kaskazini mwa Italia, kabla ya kufungua mipaka yake kwa nchi nyingi za Ulaya mwezi Juni. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kulegeza vizuizi, iliyochukuliwa na serikali wiki tatu silizopita, inakuja wakati Ulaya inashuhudia kuongezeka kwa visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona, na hivyo wengi kuwa na hofu ya mlipuko mpya wa janga hilo.

Mwezi Machi mwaka huu Berlin ilikuwa imepiga marufuku safari zote, wakati virusi vilikuwa vikiendelea kaskazini mwa Italia, kabla ya kufungua mipaka yake kwa nchi nyingi za Ulaya mwezi Juni.

Marufuku kadhaa kwa baadhi ya nchi za Ulaya yamechukuliwa kama nchini Ufaransa, na hatua kama hizo zitatumika katika siku zijazo kwa nchi nyingi duniani kulingana na vizingiti vya maambukizi.