EU-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Umoja wa Ulaya kuichukulia hatua za kisheria Uingereza

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema wameamua kutuma barua rasmi kwa serikali ya Uingereza ikiwa ni hatua ya kwanza katika mchakato wa ukiukwaji.
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema wameamua kutuma barua rasmi kwa serikali ya Uingereza ikiwa ni hatua ya kwanza katika mchakato wa ukiukwaji. Yves Herman/Reuters

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja huo umeanza mchakato wa kisheria dhidi ya serikali ya Uingereza kwa kile anachosema London imekuwa ikijaribu kukiuka baadhi ya vifungo vilivyokubaliwa katika mkataba wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyo wa EU amesema Uingereza ina mwezi mmoja kujibu mashtaka dhidi yake, ambayo huenda yakafikishwa katika Mahakama ya Haki ya Umoja huo.

Hatua hii imekuja baada ya wabunge nchini Uingereza siku ya Jumanne, kupitisha mswada utakaoiwezesha Uingereza kudhibiti soko lake kuanzia Januari tarehe 1 mwaka 2021, wakati nchi hiyo itakapojiandoa katika soko la pamoja la Umoja wa Ulaya.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema wameamua kutuma barua rasmi kwa serikali ya Uingereza ikiwa ni hatua ya kwanza katika mchakato wa ukiukwaji.

Sakata hilo la ukiukaji makubaliano ambalo linaweza kufikishwa mbele ya mahakama za Umoja wa Ulaya, halijazuia mazungumzo ya biashara ya baada ya Brexit, lakini linadhihirisha mvutano unaozidi kuongezeka baina ya pande hizo mbili kadri muda unavyoyoyoma.