UFARANSA-CORONA-AFYA

Maambukizi ya Corona yaongezeka kwa kasi katika mji wa Paris

À Paris, le port du masque est obligatoire pour fKatika mji wa Paris, kuvaa barakoa ni lazima ili kudhibiti maambukizi zaidi ya COVID-19.reiner la progression de l'épidémie de Covid-19.
À Paris, le port du masque est obligatoire pour fKatika mji wa Paris, kuvaa barakoa ni lazima ili kudhibiti maambukizi zaidi ya COVID-19.reiner la progression de l'épidémie de Covid-19. Gonzalo Fuentes/Reuters

Nchini Ufaransa, jiji la Paris, litafunga maeneo ya burudani kama vile baa kuanzia Jumanne wiki hii, hatua hii inajiri baada ya serikali ya nchini humo kutangaza kuwa maambukizi ya virusi vya corona yameanza kuongezekeza kwa kasi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Ufaransa, Jean Castex, hii leo Jumatatu anatarajiwa kutangaza masharti mengine zaidi ya kukabiliana na janga la Corona.

Siku ya Jumapili, Ufaransa ilitangaza visa vipya 12,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Siku ya Jumapili Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kwamba jiji la Paris na vitongoji vyake vya ndani (Hauts-de-Seine, Seine-Saint-Denis na Val-de-Marne) zimeingia katika eneo la tahadhari kubwa kutokana na kushika kasi kwa janga la COVID-19.

"Hatua za kujizuia", zilizopangwa kwa siku 15, zinatarajiwa kutangazwa Jumatatu hii asubuhi na Meya Anne Hidalgo.

Tishio hilo lilikuwa limetanda katika mji wa Paris na vitongoji vyake vya ndani kwa siku kadhaa. Kutokana na kuongezeka kwa janga la COVID-19, Wizara ya Mambo ya Ndani imeliambia shirika la habari la AFP Jumapili hii kwamba mji mkuu na viunga vyake vya Hauts-de-Seine (92), Seine-Saint-Denis (93) na Val-de-Marne (94), vimeingia katika eneo la tahadhari ya hali ya juu.

Matignon imeamua kwamba "hatua za kisheria" zitachukuliwa na kutangazwa Jumatatu, Oktoba 5 saa 11:30 asubuhi na Anne Hidalgo, meya wa jiji la Paris, na Didier Lallement, mkuu wa polisi wa mji huo. Hatua hizo zitaanza kutekelezwa Jumanne, Oktoba 6, kwa muda wa siku 15.