Coronavirus: Visa vipya 18,746 vya maambukizi vyathibitishwa Ufaransa
Imechapishwa:
Wizara ya afya nchini ufaransa, imetangaza maambukizi mapya 18,746 ya virusi vya Corona, idadi ambayo ni ya juu zaidi kuliko ile iliyotangazwa siku ya Jumatano ya watu 10,489.
Idadi ya watu waliofariki nchini humo kutokana na janga la Corona sasa imefikia zaidi ya laki sita na hamsini, hatua ambao rais Emmanuel Macron amsema huenda ikalazimu kuwekwa kwa makataa mapya ya kudhibiti maambukizi zaidi.
Hivi karibuni Ufaransa iliagiza kufungwa kwa vilabu vya kuuza pombe na mikahawa mjini Marseille na kudhibiti biashara hiyo katika maeneo ya jijini la Paris ili kusaidia kupambana na janga la Corona.
Hatua hii ilikuja baada ya nchi hiyo ya bara Ulaya kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona kuanzia mwezi Agosti na kutangaza kudhibiti mikusanyiko ya watu katika maeneo ya umma.
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex alitoa wito kwa wananchi wa Ufaransa kuwa na "nyoyo za uwajibikaji" kwa kuvaa barakoa, jambo ambalo 'ni muhimu sana' katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19.