UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 4,500 za maambukizi zathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 314,660, baada ya visa vipya zaidi ya 4,516 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kito cha kuzuia na kutbiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni. AFP/Torsten Silz
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na RKI, vifo vipya kumi na moja vimeripotiwa, na kufikisha jumla ya vifo 9,589 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.