UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Johnson kutangaza vizuizi vipya Jumatatu

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. PRU / AFP

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajia kulihutubia Bunge huko Westminster Jumatatu ambapo atangaza hatua masharti mapya ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

"Kuongezeka kwa kiwango cha matukio katika maeneo mengine kunamaanisha kuwa kuna uwezekano kwamba maeneo mengine yatakuwa chini ya masharti zaidi," Edward Lister, mshauri wa waziri mkuu, amesema katika barua kwa wabunge.

"Serikali inatarajia kumaliza utaratibu huu haraka iwezekanavyo. Ratiba hii ni muhimu ikiwa tunataka kudhibiti kusambaa kwa virusi," ameongeza.

Kwa wastani, idadi ya kila siku ya visa vya maambukizi nchini Uingereza iliongezeka maradufu katika wiki moja mwishoni mwa mwezi uliopita, kulingana na utafiti wa Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa (ONS) iliyotolewa Ijumaa, lakini serikali inakabiliwa , kama ilivyo katika nchi nyingine za Ulaya, na ongezeko la visa vya maambukizi.