USWISI-MALI-USALAMA

Mali: Mmishonari wa Uswisi, aliyeshikiliwa mateka, auawa na watekaji nyara

Mji wa Timbuktu, Mali, Januari 16, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Mji wa Timbuktu, Mali, Januari 16, 2020 (picha ya kumbukumbu). Souleymane Ag Anara/AFP

Mateka mwingine nchini Mali, mwanamke wa Uswisi, ameuawa na watekaji nyara waliokuwa wakimshikilia. Bern imetangaza rasmi Ijumaa, Oktoba 9, jioni. Hatujui kwa sasa ikiwa kifo chake kina uhusiano na kuachiliwa kwa Soumaila Cissé na Sophie Pétronin.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Uswisi hatangaza jina la mateka huyo ambaye anadaiwa kuuawa, mwandishi wetu huko Geneva, Jérémie Lanche, ameripoti. Mmishonari huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye alizaliwa Basel, alitekwa nyara miaka minne iliyopita huko Timbuktu na kundi lenye mafungamano na al-Qaeda.

Aliwahi kutekwa nyara kwa muda mfupi mwaka 2012, wakati mji huo ulianguka mikononi mwa wanajihadi. Alionekana kwenye video ya watekaji nyara mwaka 2017, huku akionekana kuwa ni mdhaifu na amekonda.

Mmishonari huo aliuawa mwezi mmoja uliyopita. Sophie Pétronin, mateka wa Ufaransa aliyeachiliwa hivi karibuni nchini Mali, ambaye aliwasili nchini Ufaransa jana Ijumaa ndiye alitoa taarifa kuhusu kifo chake kwa mamlaka nchini Ufaransa. Waziri wa mambo ya Nje wa Uswisi, Ignazio Cassis, amelaani kile alichokiita "kitendo cha kikatili" na ametoa "rambi rambi kwafamilia ya marhemu".

Duru za kuaminika zinabaini kwamba mmishonari huyo "aliuawa na watekaji nyara wa kundi la kigaidi la Kiislamu la Jama'at Nasr al-Islam wal Muslim". Uswisi sasa inatafuta kujua mazingira halisi ya kifo cha raia wake, na pia wapi ulipo mwili wake.