UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 4,100 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu. Ina FASSBENDER / AFP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 329,453, baada ya visa vipya 4,122 kuripotiwa siku moja liyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumanne na Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na RKI, vifo vipya kumi na tatu vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,634 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.