Mazungumzo ya baada ya Brexit yaingia katika hatua muhimu
Imechapishwa:
Viongozi wa mataifa ya Ulaya wanatarajia kuaandaa kikao hii leo kujadili kuhusu kujiondoa kwa baadhi ya mataifa katika Umoja wa Ulaya, wakati huu Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiendelea kutoa shinikizo la Uingereza kujiondoa katika umoja huo bila ya vikwazo.
Viongozi ishirini na saba kutoka katika mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wameonekana kujaribu kulikwepa swala hilo, lakini shinikizo za Boris Johnson ni kuondoa nchi yake katika umoja huo iwapo suluhisho halitapatikana katika mazungumzo hayo ya siku siku mbili.
Jumatano wiki hii maafisa wakuu wa Umoja wa Ulaya walimuelezea Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuwa wataendelea na mazungumzo ya biashara ya baada ya Brexit lakini hawataweka rehani maslahi ya kanda ya Ulaya.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel na mwenzake wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo Ursula von der Leyen wamemfahamisha Johnson kuwa umoja huo unalenga kufikia mkataba lakini chini ya masharti yanayolinda maslahi yake.
Maafisa hao wamesema ni lazima kuwepo misimamo inayokubalika katika masuala tete yanayokwamisha kupiga hatua kwa mazungumzo yanayoendelea hususan suala la sekta ya uvuvi na ushindani wa kibiashara.