UFARANSA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ufaransa yakumbwa na maambukizi zaidi

Maafisa wa polisi wa Manispaa wakipiga doria Colombes, karibu na jiji la Paris, Machi 22, 2020 wakati wa kizuizi kwa raia cha kutotembea.
Maafisa wa polisi wa Manispaa wakipiga doria Colombes, karibu na jiji la Paris, Machi 22, 2020 wakati wa kizuizi kwa raia cha kutotembea. FRANCK FIFE / AFP

Ufaransa imeripoti  idadi ya juu ya maambukizi ya Corona, siku moja tu kabla kuanza kutekelezwa masharti mapya yaliyotangazwa na rais Emmanuel Macron siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Rais Macron siku ya Jumatano alitangaza masharti mapya, yakiwemo maarufuku ya kutotembea kwenye miji minane ikiwemo jiji kuu la Paris, lengo likuwa kupunguza maambukizi ya kila siku kwa visa elfu tatu.

Aidha kwenye mpango huo wakaazi wa miji hiyo watahitaji kupata kibali cha kuwa nje ya nyumba zao.

Hata hivyo maambukizi ya virusi vya Corona yameongezeka kwa visa zaidi ya elfu 30 ndani ya siku moja .

Shirika la Afya Duniani, WHO,  limeonya kuwa kutokana na mlipuko huo wa pili wa virusi vya Corona, masharti makali ya kudhibiti yanahitajika ili  kuokoa maisha ya watu.

Mataifa mengine  ambayo yameshuhudia ongezeko la kasi  la virusi vya Corona ni Italia, Poland  na Ujerumani, huku Urusi ikiendelea kuripoti idadi ya  juu ya  vifo  kutokana na Corona.