UFARANSA-UGAIDI

Mauaji ya mwalimu Ufaransa: Mshambuliaji aliwadadisi wanafunzi kabla ya kumuua

Watu 5 zaidi wakamatwa na polisi kuhusiana na mauaji ya mwalimu Ufaransa
Watu 5 zaidi wakamatwa na polisi kuhusiana na mauaji ya mwalimu Ufaransa ABDULMONAM EASSA / AFP

Mtu aliyehusika kumchinja mwalimu raia wa Ufaransa mwishoni mwa juma hili, anadaiwa aliwasubiri wanafunzi kutoka nje ya shule na kuwataka wamtambue mwalimu huyo, imesema taarifa ya ofisi ya kupambana na ugaidi nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Baadae mtu huyo anadaiwa alichapisha kwenye mitandao ya kijamii, picha ya mwalimu aliyemuua, Samuel Paty, ambaye aliwaonesha wanafunzi wake kibonzo chenye utata kumuhusu Mtume Muhammad. 

Taarifa ya ofisi hiyo imedai kuwa mtuhumiwa baadae aliwafyatulia risasi polisi kabla yay eye kuuawa. 

Hadi sasa idadi ya washukiwa waliokamatwa kuhusiana na tukio hili imefikia 10, wakati huu polisi wakichunguza ikiwa tukio hili lina uhusiano na masuala ya itikadi kali. 

Tukio hili lilitekelezwa siku ya Ijumaa, maajira ya saa kumi na moja jioni jinari na chuo cha Du Bois d’Aumne, ambako mwalimu Paty alikuwa akifundisha. 

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema shambulio hili lina kila ishara ya uhusiano na masuala ya itikadi kali na ugaidi, na kwamba mwalimu huyo aliuawa kwa sababu tu ya kuwafundisha wanafunzi wake uhuru wa kujieleza. 

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Jean-Francois Ricard, amemtaja mtuhumiwa kuwa ji Abdoulakh A mwenye umri wa miaka 18, aliyezaliwa mjini Moscow na mwenye asili ya watu wa Chechen. 

Ricard, anasema mtuhumiwa aliingia nchini Ufaransa na kupewa kibali cha kuishi kama mkimbizi na alikuwa akifahamika na idara ya makachero waliokuwa wakimfuatilia. 

Taarifa imeongeza kuwa, mtuhumiwa alienda chuoni hapo Ijumaa mchana na kuanza kuwauliza wanafunzi kuhusu mwalimu huyo. 

Baadae inadaiwa alimfuata mwalimu Paty aluyekuwa akirejea nyumbani kwa mguu, ambapo alianza kwa kumshambulia kichwani kwa kitu chenye ncha kali na kumjeruhivibaya kabla ya kumchinja. 

Mashuhuda wamedai kuwa walisikia sauti ya mtu akitamka maneno ya Ammahu Akbar ‘’Mungu Mkubwa’’