POLAND-CORONA-AFYA

Coronavirus: Poland yatenga hospitali ya muda Warsaw baada ya maambukizi zaidi

Serikali ya Warsaw wiki iliyopita iliwasihi wananchi wake kukaa nyumbani, na kuamuru kufungwa kwa sehemu za kufanyia mazoezi kuogelea, huku migahawa ikitakiwa kufungua kwa masaa kadhaa.
Serikali ya Warsaw wiki iliyopita iliwasihi wananchi wake kukaa nyumbani, na kuamuru kufungwa kwa sehemu za kufanyia mazoezi kuogelea, huku migahawa ikitakiwa kufungua kwa masaa kadhaa. REUTERS

Poland, ambapo mfumo wa afya umezidiwa na wimbi jipya la janga la Corona, inatarajia kutenga hospitali ya muda kwenye uwanja wa Warsaw baada ya kuripotiwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona, serikali imesema.

Matangazo ya kibiashara

Poland imeweka rekodi za maambukizi mapya na vifo katika wiki za hivi karibuni na madaktari wanakosa wafanyakazi, vitanda na vifaa vya kukabiliana na wingi wa wagonjwa wa Covid-19."

Jumamosi, Waziri Mkuu aliamuru kuanzishwa kwa hospitali ya kwanza ya muda, ambayo itawekwa katika uwanja wa kitaifa", katibu mkuu wa serikali, Michal Dworczyk, alitangaza kwenye Redio Zet.

Vitanda mia tano kwa wagonjwa wa Covid-19 vitawekwa mwanzoni na baadaye kuongezeka hadi vitanda 1,000, alisema.

Serikali ya Warsaw wiki iliyopita iliwasihi wananchi wake kukaa nyumbani, na kuamuru kufungwa kwa sehemu za kufanyia mazoezi kuogelea, huku migahawa ikitakiwa kufungua kwa masaa kadhaa.

Siku ya Jumamosi, Poland iliripoti maambukizi mapya 9,622 na katika muda wa asaa 24. Idadi ya vifo imefikia 3,524 na maambukizi 167,230 yaliyothibitishwa.