UBELGIJI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ubelgiji yakabiliwa na ongezeko la maambukizi

Katika jaribio la kudhibiti mlipuko huu mpya, serikali ya ubelgiji imeagiza baa na mikahawa ifungwe kwa wiki nne. Sheria ya kutotoka nje pia imeanza kutumika leo Jumatatu.
Katika jaribio la kudhibiti mlipuko huu mpya, serikali ya ubelgiji imeagiza baa na mikahawa ifungwe kwa wiki nne. Sheria ya kutotoka nje pia imeanza kutumika leo Jumatatu. REUTERS

Hali ya sasa ya kiafya nchini Ubelgiji ni mbaya kuliko ile ya mwezi Machi na rekodi za kila siku za maambukizi ya virusi vya Corona na kuongezeka mara mbili kwa kila wiki kwa idadi ya watu wanaolazwa hospitalini, mamlaka imesema.

Matangazo ya kibiashara

"Hali ni mbaya. Ni mbaya zaidi kuliko ile ya mwezi Machi 18, wakati tuliamua kweka masharti ya watu kutotembea," Waziri Mkuu Alexander De Croo ameonya kwenye kituo cha runinga cha RTL-Info.

Katika jaribio la kudhibiti mlipuko huu mpya, serikali imeagiza baa na mikahawa ifungwe kwa wiki nne. Sheria ya kutotoka nje pia imeanza kutumika leo Jumatatu.

Idadi ya wagonjwa katika vitengo vya wagonjwa mahututi, iliyofikia 412 jana Jumapili, inaongezeka mara mbili kila baada ya siku nane hadi tisa na nusu ya wagonjwa hao wanatumia vifaa maalum kwa kupumua, mamlaka imebaini.

Idadi ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini huongezeka mara mbili kila wiki. Oktoba 17, watu 351 walilazwa hospitalini, zaidi ya nusu ya idadi iliyorekodiwa mnamo Machi 28 ambayo ilifikia wagonjwa 629.

Msemaji wa wizara ya afya Yves Van Laethem amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba idadi ya wagonjwa katika wodi za wagonjwa mahututi itaongezeka hadi zaidi ya 500 wiki hii.