IRLAND-CORONA-AFYA

Covid-19: Ireland yaweka masharti mapya kukabiliana na ongezeko la maambukizi

Ongezeko la kimataifa la maambukizi la wiki za hivi karibuni limekuwa likishuhudiwa zaidi barani Ulaya, ambako zaidi ya watu 240,000 wamefariki kutokana na janga hilo hadi sasa.
Ongezeko la kimataifa la maambukizi la wiki za hivi karibuni limekuwa likishuhudiwa zaidi barani Ulaya, ambako zaidi ya watu 240,000 wamefariki kutokana na janga hilo hadi sasa. REUTERS

Raia wa Ireland wametakiwa kubaki makwao kuanzia usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi ili kukabiliana na janga la Covid-19. Ireland inakuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuchukua hatua hiyo, Waziri Mkuu wa Irland Micheal Martin amesema.

Matangazo ya kibiashara

Makataa hayo mapya yataanza kutumika Jumatano saa sita usiku kwa kipindi cha wiki sita, amesema Micheal Martin, huku akibaini kwamba shule zitaendelea na shughuli zao.

Kwa upande mwingine, biashara ambazo sio muhimu zitalazimika kufungwa.

Ongezeko la kimataifa la maambukizi la wiki za hivi karibuni limekuwa likishuhudiwa zaidi barani Ulaya, ambako zaidi ya watu 240,000 wamefariki kutokana na janga hilo hadi sasa.

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imepindukia milioni 40 kote ulimwenguni. Kulingana na Chuo Kikuu cha John Hopkins ambacho kinakusanya takwimu kutoka kote duniani, idadi hiyo ilipindukia hapo jana. Aidha wataalamu wamesema idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo.

Hadi sasa, zaidi ya watu milioni 1.1 wamefariki kutokana na virusi vya corona, ingawa wataalamu pia wanaamini idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo. Marekani, India na Brazil ndiyo mataifa yanayoripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ulimwenguni kote.