UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Masharti mapya yatangazwa Kaskazini mwa Uingereza

Maeneo ya kaskazini mwa Uingereza yameathiriwa vibaya na mlipuko mpya wa COVID-19.
Maeneo ya kaskazini mwa Uingereza yameathiriwa vibaya na mlipuko mpya wa COVID-19. REUTERS/Toby Melville

Eneo la South Yorkshire, kaskazini mwa Uingereza, litawekwa kwenye kiwango cha "juu zaidi" cha hatari siku ya Jumamosi katika jaribio la kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, meya wa mkoa wa Sheffield Dan Jarvis amesema leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mpango wa msaada unaofikia pauni milioni 41 (sawa na euro milioni 45.1) utatolewa na mamlaka ya jimbo kwa makampuni ambayo yatalazimika kufunga milango pamoja na ufadhili wa hatua za ziada za afya ya umma.

Maeneo ya kaskazini mwa Uingereza yameathiriwa vibaya na mlipuko mpya wa COVID-19 ambao kwa sasa unazikumba nchi nyingi za Ulaya. Na jimbo la South Yorkshire liitajiunga na majimbo ya Liverpool na Lancashire, ambayo tayari yameingia kwenye kiwango cha juu cha tahadhari.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Jumanne kwamba jimbo la Manchester, kaskazini magharibi mwa Uingereza, pia litawekwa kwenye tahadhari "kubwa zaidi", baada ya kushindwa kwa mazungumzo na viongozi wa eneo hilo juu ya mpango wa msaada kifedha.