UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yapindukia zaidi ya 400,000 Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. Ina FASSBENDER / AFP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya mambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 403,291, baaada ya visa vipya 11,242 kuthibitishwa siku iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kituo cha kuzuia na kudhibiti magojnwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya 49 vimeripotiwa na RKI, na kufanya jumla kufikia 9,954 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Juzi Jumatano Ujerumani ilirekodi kwa mara ya kwanza zaidi ya visa vipya 10,000 vya maambukizi kwa siku moja, na kusababisha mamlaka kuwa na wasiwasi.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.